Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media, Dar es Salaam
Jeshi la Magereza limewashauri maelekezo wazazi/Nlndugu jamaa na marafiki wa vijana ambao walikamatwa Oktoba 29,30,2025 na wamekwisha fikishwa mahakamani kufika mahabusu kuwaona ndugu zao ikiwemo kuwapelekea mavazi na mahitaji mengineyo .
Itakumbukwa 7, Novemba, 2025 mashauri yanayohusisha kula njama ya kufanya kosa la jinai, uhaini, uharibifu wa mali, unyang’anyi wa kutumia silaha, uchomaji wa mali na kufanya maandamano bila vibali yalifunguliwa na Jamhuri katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mara, Mwanza, Arusha, Njombe na Kigoma. Watuhumiwa wengi wa makosa haya ni vijana wenye umri kati ya
miaka 19 mpaka 25 walifikishwa mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari November 11,2025 Jijini Dar es salaam Wakili Dicksoni Matata kutoka CHama cha Mawakili Tanganyika(TLS) amesema baadhi ya ndugu wameendelea kuwa na Mashaka na Kutumia fedha kutafuta ndugu zao pasipo matumaini hivyo kumbe wengine walikuwa wamekamatwa na kupelekwa mahabusu kwa tuhuma mbalimbali bila taarifa kufikishiwa ndugu zao hivyo ni vyema mtuhumiwa akapewa nafasi ya kutoa taarifa kwa ndugu zake ili wasikae na hofu
“Baada ya mashauri haya kuanza kufunguliwa tulikaa na kufanya tathimini ambapo tulibaini kuwa watuhumiwa walio wengi uelewa wao wa kisheria ni mdogo na wengi hawana hata uwezo wa kulipia gharama za mawakili kwa ajili ya kuwawakilisha kwa mujibu wa Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977″Amesema Wakili Dicksoni
Hivyo mawakili kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) wameamua kujitolea kutoa msaada wa kisheria ikiwemo kuwawakilisha mahakamani watuhumiwa wote waliofikishwa mahakamani tangu tarehe 7 na ambao wataendelea kufikishwa mahakamani siku hadi siku bila malipo na bila masharti yoyote.

Naye Wakili Maduhu Willium amesema idadi ya watuhumiwa waliokuwa wanashikiliwa katika mahabusu mbalimbali kote nchini inakadiriwa kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam pekee zaidi ya watu 400 walikamatwa, Mwanza 200 walikamatwa, Kilimanjaro takribani watu 312 , Kilimanjaro watuhumiwa 300 wamekwisha achiwa na 12 bado wanashikiliwa huku taratibu za kiupelelezi zikiendelea dhidi yao. Mkoa wa Tabora ,watuhumiwa 5 wanashikiliwa na , Mbeya 300, Njombe watuhumiwa zaidi ya 10 pia, Songwe 200,,Kigoma zaidi ya 10


