Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,
Dar es Salaam
NGOME ya Vijana Taifa ACT Wazalendo imewashauri watawala wanaopa kwa Kutumia vya vitabu vya dini kwa imani zao ambavyo pia vimeagiza kudumisha haki . Qur’an katika surat An-Nahl aya ya 16:90, Mungu anaagiza waja wake kutenda haki, usawa na matendo mema na Biblia ukisoma Isaya 1:17 inasema “Jifunzeni kutenda mema, tendeni haki, ondoeni udhalimu”.
Watawala wanaapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ambayo kuanzia ibara ya 12 hadi 24 zinazungumzia HAKI,HAKI, HAKI, HAKI kama msingi wa amani na utulivu hivyo kufuatia tukio la 29 ,30Oktoba 2025 limeongeza chuki na uhasama hivyo ni budi Kutumia busara na hekima kujitokeza kuzungumza ili kuliponya Taifa,kuliunganisha na kutengeneza Nchi yenye haki na usawa.
Akizungumza November 12,2025 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Abdul Nondo amesema ni vyema sote kama nchi bila kuangalia itikadi za kivyama kidini kujiulize kwa uaminifu na moyo uliojaa majonzi tumefikaje hapa?.Tukijibu swali hili kwa uaminifu,uwazi na ukweli ndipo
tutapata jibu la tunatokaje hapa tulipo ili kuirejesha Tanzania yenye upendo, umoja, ukarimu, utu, amani.
“22 Oktoba, 1987 Mwl. Nyerere akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 3 wa CCM alisema ‘Kila kilichoundwa,kisipotunzwa huharibika. Msingi wa amani ni haki ama haki yenyewe kama ipo au matumaini ya kujenga Taifa lenye haki. Panapokuwa hapana haki wala imani ya matumaini ya kupata haki hapawezi kuwa na amani na utulivu wa kisiasa’. Watawala wana wajibu mmoja tu sasa ni kujenga Taifa lenye HAKI ili amani na utulivu wa nchi yetu idumu” amesisitiza Nondo.


