Rais Samia Suluhu Hassan leo amewasilisha bungeni jina la Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Spika Mussa Zungu alipokea hati ya uteuzi huo kutoka kwa Rais Samia na kulijulisha kwa wabunge kwa ajili ya kumthibitisha kwa kura kwa mujibu wa Ibara ya 51 kifungu kidogo cha cha pili cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hati ya jina lake limewasilishwa leo Bungeni Jijini Dodoma Novemba 13, 2025, na Mpambe na Mshauri Masuala ya Kijeshi wa Rais, Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri ikiwa ndani ya bahasha kisha kufunguliwa na Spika wa Bunge Mwigulu anakuwa Waziri wa 12 tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania.
Mwigulu ni mchumi, kada wa muda mrefu wa chama cha mapinduzi, (CCM) akimrithi Kassim majaliwa anayemaliza muda wake. Mwanasiasa huyo wa muda mrefu, alikuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Samia.


