Jeshi la Polisi nchini Tanzania lingependa kujulisha kuwa, lilimkamata na linaendelea kumshikilia Ambrose Leonce Dede, Mnyaturu, Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya African Safari na Mwanachama wa Chama cha Chadema kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha uhalifu nchini kupitia kundi la whatsApp lijulikanalo kwa jina la SAUTI YA WATANZANIA.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa maeneo ya njia panda ya Makiungu Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Kulingana na ushahidi uliokusanywa kabla na baada ya kukamatwa kwake, unaonyesha katika kundi hilo yupo pamoja na wasimamizi wengine wa kundi hilo la whatsApp (Group Admin’s) na wanashirikiana na baadhi ya watu waliopo nchini na wengine wakiwa nje ya mipaka ya nchi yetu.
Alioshirikiana nao kupanga, kuendelea kupanga na kuhamasisha uhalifu nchini kwa mwavuli wa maandamano ya amani ni pamoja na wanaotumia namba zifutazo;
- +44746913055
- +46732533609
- +1(240)423-3331
- +44784821186
- +1(649)9348015
- +255758000000
- +255655684245
Uchunguzi unakamilishwa ikiwa ni pamoja na kuwapata wengine anaoshiriana nao na wanatumia namba ambazo hatujazitaja kwasababu za kiuchunguzi na ukamataji. Baada ya kukamilisha hayo hatua zingine za kisheria zitafuata.
Jeshi la Polisi, linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujihusisha na makundi ya mawasiliano mtandaoni yanayoendeshwa na watu waliopanga na wanaendelea kupanga kufanya uhalifu nchini kwa mwavuli wa maandamano ya amani au kwasababu nyingine yeyote ile kwani huo ni uhalifu na hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria bila kumwonea muhali yeyote yule atakayebainika.
Aidha, ni vizuri kila mmoja wetu kutambua kuwa, watu wa aina hiyo wanaopanga na kuhamasisha uvunjifu wa amani, wanaoumia ni sisi Watanzania wakati wao na familia zao hawapati madhara yoyote na wanaendelea kunufaika na fedha wanazolipwa kupitia makundi ya mawasiliano mtandaoni wanayoyaanzisha na kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.
Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania

