WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Nishati mara baada ya uapisho uliofanyika Novemba 18, 2025.

Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba.