Na Mwandishi wetu,JamhuriMedia
Dar es Salaam
Maridhiano,Maridhiano mara baada ya Uchaguzi Oktoba 29,2025 imekuwa gumzo kubwa linalozungumzwa kila Kona ya Tanzania na CHama Cha Tanzania labour Part TLP kimeshauri Vyama vya vyote na Viongozi wa Dini na Wadau Mbalimbali kuketi meza moja kuzungumza na kufikia muafaka wa pamoja utakoendeleza Amani na Utulivu
Ameyasema hayo November 21,2025 Dar es salaam Mwenyekiti wa TLP Richard Lyimo ambapo ameabaisha kuwa Wakati wa Uchaguzi illitokea Vurugu katika Maeneo Mbalimbali ambapo ilileta taharuki hivyo kwakuwa Uchaguzi umekwisha tushirikiane tujenge Uchumi wetu Imara hivyo
” Yaliyopita si ndwele turudi tukae meza moja tuzungumze tunie mamoja kwani Uchumi hauwezi kujengwa pasipo amani hivyo kama Rais amewaita wote turudia kwenye Maridhiano Vyama vyote vya Upinzani na CHama tawala ili kusaidia kuendeleza pale tulipoishia” Amesema Mwenyekiti
Hata hivyo amewaomba Vyama vyote vya siasa wote kuangalia UTu na Amani ya MTanzania hao Vijana wanahamasisha kwenye mtandao kwamba Desemba 9,2025 kuandamana hivyo acheni kama kuna tatizo litekebishwe Kupitia mamzungumzo
Aidha Mwenyekiti amewapongeza wote waliopata nafasi Mbalimbali ikiwemo Mawaziri kufanya majukumu yao vizuri Kwa kutatua Changamoto za Wananchi ili kuleta Maendeleo kwa Taifa.

