Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassan amewasili katika kiwanja Cha  ndege Cha Kimataifa Cha Kilimanjaro (KIA) na kupokelewa na viongozi mbalimbali, tayari kuelekea Mkoani Arusha ambapo kesho Novemba 22, 2025, atatunuku Kamisheni Kwa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli.