Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Judithi Kapinga ameitaka Tume ya Ushindani FCC kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ufanisi ili kusaidia kudhibiti bidhaa feki zisifike kwa Wananchi.
Agizo hilo amelitoa meo Novemba 24,2025 Jijini Dar es Salaam katika ziara yake mara baada ya kuteuliwa ambapo amesema kikao hicho kimeangazia namba nzuri ya utendaji kuweza kudhibiti bidhaa feki kwa kuwekeana mikakati itakayoweza kuwafikisha katika mlengo waliyokusudia kumkinga Mwananchi dhidi ya bidhaa zisizo na ubora .

“Tume hii ya Ushindani ni muhimu Sana kwa mustakabali wa Taifa letu kwani Lina jukumu kubwa kwenye masuala ya Udhibiti bidhaa feki ,kulinda walaji,Elimu kwa Umma pamoja na masuala mengine ya kibiashara ikiwemo Biashara Muunganiko na makampuni Makubwa ili kuhakikisha inakuwa shindani wenye manufaaa na kuweka ustahimilivu wa Biashara” amesema Waziri Kapinga
Hata hivyo amebainisha kuwa ulimwengu wa sasa ni wa tofauti sana na mazingira ya kibiashara yanayotofautiana hivyo wameweka mikakati mizuri kuongeza ufanisi, ubunifu,weledi na kushirikiana na sekta binafsi.
Hivyo Kapinga ameipongeza FCC kwani imekuwa ikitekeleza majukumu yake vizuri sana na matokeo mengi ambavyo yanaonekana kwenye jamii ni kwa sababu ya uwajibikaji.

Kwa Upande wake Kamu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani FCC, Khadija Juma Ngasongwa amesema tume inakwenda na falsafa ya Rais ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha vyombo hivi kutatua matatizo ya wananchi haswa katika ufanyaji wa biashara
kupitia marekebisho ya sheria yaliyopitishwa na Bunge, tume imeweka vifungu maalum vinavyolinda na kutetea haki za mlaji, hasa pale anapopata usumbufu au madhara kutokana na bidhaa zisizokidhi viwango.
Hadija Kasongwa amebainisha kuwa miaka hii minne kulikuwa na falsafa ya ukuzaji uwekezaji nchini na wao kama taasisi wanapitia na kuchambua miamala ya miunganiko ya makampuni kwa lengo la kukuza mitaji pamoja na kuokoa ajira ambazo kwa baadhi ya kampuni na viwanda.

Sisi tunafahamu watanzania wanatufahamu sana na watanzania ndio wateja wetu ndio walaji hivyo kikao cha leo kinalenga kabisa namna nzuri ya utendaji kazi ili kufikia mategemeo ya watanzania ambao ni walaji pamoja na kuongeza njia ambayo tutawafikia zaidi ili kuweza kupata mrejesho wa kazi tunazozifanya kwa urahisi zaidi” Bi Khadija
Aidha tume imeweka mfumo unaozingatia falsafa tatu—kurekebisha (repair), kubadilisha (replace) na kurejesha fedha (refund)—kwa bidhaa zinazolalamikiwa. “Endapo mlaji atashindwa kupata suluhu dhidi ya mtoa huduma, FCC huingilia kati kwa utaratibu wa kimahakama. Tumetenga siku maalum za kusikiliza malalamiko katika ngazi ya kamati ili kuhakikisha mlaji anasikilizwa moja kwa moja,” alieleza.






