Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa mwaka mmoja kwa wananchi wote waliotumia nyaraka za kughushi au waliotoa taarifa zisizo sahihi wakati wa usajili.
Lengo ni kuwawezesha wale wote wenye chngamoto .kufanya marekebisho na
kufanya usajili sahihi kuanzia kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia Oktoba
2025.
Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa habari ,Mkurugenzi mkuu wa
(NIDA) James Kaji amesema kumekuwa na maombi ya mbalimbali ya mabadiliko ya taarifa kwa muda mrefu, lakini hayakuweza kufanyiwa kazi, kutokana na kutokidhi matakwa na utaratibu uliokuwa unatumika
hapo awali.
Kaji amesema kati ya maombi ambayo ,hayakuweza kufanyiwa kazi ni ya watu waliotumia nyaraka za kughushi pamoja na waliotoa taarifa za udanganyifu walipojisajili NIDA.
‘’Kufuatia hali hiyo, Serikali imetoa kibali maalum kwa ajili ya kushughulikia maombi ya mabadiliko ya taarifa ambayo awali hayakuweza kufanyika kutokana na kukinzana na miongozo inayosimamia mabadiliko ya
taarifa.

Kibali hiki maalum, kimetolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Oktoba 2025 na zoezi hili litafungwa baada ya muda huo kuisha.
Aidha kibali hiki kitahusisha, waathirika wa vyeti vya kughushi, waliofukuzwa katika ajira za Serikali kutokana na kutumia vyeti vya
shule vya kughushi
Wengine walitumia vyeti hivyo, kujisajili NIDA,watu waliotumia majina ya watu wengine kupata vyeti vya elimu , watu waliotoa taarifa za uongo/udanganyifu katika usajili wa NIDA’’amesema.
Amesema Raia wa Tanzania waliojisajili kama qakimbizi, na makundi haya manne, kufika katika Ofisi za NIDA za Wilaya wakiwa na nyaraka zinazohitajika kulingana na changamoto iliyopo ili iwe rahisi
kushughulikia maombi ya mabadiliko hayo.
Aidha, amedai watu hao watalazimika kuwa na viambatisho vya lazima pamoja na vya ziada kama watakavyo elekezwa.
Naendelea kuwasisitizia wananchi kuwa, maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale tu yatakayokidhi masharti na vigezo vilivyowekwa baada ya wahusika kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa kwa ajili ya kuthibitisha
taarifa zao.
Kwa kuwa kibali hiki kimetolewa kwa muda maalum, niwaase wale wote wenye changamoto za taarifa hizo, kujitokeza na kwenda kwenye ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na viambatisho vinavyotakiwa ili kufanya marekebisho wanayohitaji katika muda uliopangwa’’.amesema
Sambamba na hilo, Kaji amewakumbusha wananchi wote kutoa taarifa sahihi na za ukweli wanapokuja kujisajili NIDA kwa ajili ya
Utambulisho wa Taifa,
Amesema kutoa taarifa zisizo sahihi au kufanya udanganyifu wa taarifa eakati wa usajili ni kosa, kwa mujibu wa Sheria ya Usajili na utambuzi wa watu.
Kaje amedai matarajio ya NIDA ni kuwataka wananchi wenye changamoto zilizotajwa kutumia fursa hii kufanya marekebisho kama ilivyoelekezwa kwenye kibali kabla ya muda kwisha
