KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV alihimiza mshikamano na matumaini mapya katika Lebanon inayokabiliwa na migogoro akipongeza ‘ustahimilivu’ wa nchi hiyo licha ya miaka ya migogoro na misukosuko.

Katika sehemu ya pili ya ziara yake ya kwanza ya nje, baada ya kusimama nchini Uturuki, Papa alikutana na Rais wa Lebanon Joseph Aoun na maafisa wakuu katika ikulu ya rais jijini Beirut.

Kiongozi huyo alisikika akisema heri wapatanishi wale wanaochagua amani hata pale migogoro inapokuwa rahisi. Kabla ya ziara hiyo, mabango kwenye barabara zilizokarabatiwa yalimkaribisha Leo kama ‘Papa wa Amani.

Na tayari ametangaza nia yake ya ‘kutangaza tena ujumbe wa amani katika Mashariki ya Kati’ na kuimarisha jumuiya za Kikristo kote katika eneo hilo.