“Lililotokea (vurugu za Oktoba 29) ni tukio la kutengenezwa na walilolitengeneza walidhamiria makubwa, walidhamiria kuangusha dola ya nchi hii..”

“Ukiangalia clip videos za nyuma zilizotokea, vijana wetu walifanywa makasuku na kuimbishwa kabisa yaliyotokea Madagascar yatokee na hapa, lakini ukimvuta kijana yule mwambie emvu niambie Madagascar kulitokea nini..hajui..unataka hapa kitokee nini, hajui..lakini waliimbishwa wimbo huo”

“Kwa hiyo lile lilikuwa ni jambo la kupangwa na vurugu zile zilidhamiria makubwa”

“Vurugu zile ni mradi mpana sana wenye nia kuu ya uovu ulio na wafadhili, washili na watekelezaji”

“Katika vurugu zile waliingia waliokuwemo na wasiokuwemo , wengine kwa kutokujua, wengine kwa kufuata mkumbo, wengine kwa hadaa za maisha bora baadaye lakini wengine kwa kulipwa tu, tunaambiwa kuna vijana walikuwa wanalipwa fedha ukishachukua fedha yako ingia barabarani kwahiyo waliingia bila madhumuni maalum ya nini wanakwenda kukifanya”

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo Disemba 2, 2025 wakati alipokutana na kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa JNICC Jijini Dar es Salaam.