Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป amehoji juu ya maoni ya baadhi ya watu kuwa nguvu zilizotumika kwenye kudhibiti vurugu zilizotokea Oktoba 29 (iliyokuwa siku ya uchaguzi mkuu) na kuendelea ilikuwa ni nguvu kubwa, akiuliza nguvu ndogo ambayo ingeweza kutumika ni ipi ambapo pia amesema dola haipo hivyo kwa kuwaacha baadhi ya vikundi vya watu kufanya vurugu na kuhatarisha amani ya Nchi.
Rais Dkt. Samia amesema Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza itahakikisha inailinda nchi na raia wake pamoja na mali zao kwa nguvu zote.
“Serikali ina wajibu, tunaapa kuilinda nchi hii, kulinda usalama wa raia na mali zake na katika hali hiyo nguvu inayotumika inaendana na tukio lililopo,”
“Sasa tunapoambiwa kwamba tulitumia nguvu kubwa sana kwenye tukio lile, nguvu ndogo ilikuwa ni ipi ilikuwa tuwaangalie waandamanaji waliojiandaa kufanya mapinduzi na vurugu mpaka wafanikiwe ?..”
Akiweka mkazo juu ya kuilinda nchi, Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa serikali itafanya kila linalowezekana kadiri ya nguvu inayotumika kuharibu amani ili kuweza kumpambana na kulinda nchi, raia na mali zao.
“..dola haipo hivyo, haya mambo si Tanzania peke yake tulishashuhudia kwa wenzetu waandamanaji wengi wanaingia njiani na wakiingia njiani serikali ikiona huu uandamanaji unaenda pasipo (kwa maana ya kuanzisha vurugu) serikali inaweka nguvu kubwa โฆyameshafanyika kwenye mataifa huko na tumeyaona”
“..wanapoalumu kuwa tulitumia nguvu kubwa, wao walitaka nini ? tujiulize je? hao ndio wafadhili wa kile kichofanyika ?, “
“..walitaka wafanikiwe waliowapa fedha, walichowatuma..hapana, tuliapa kuilinda nchi hii na mipaka yake, usalama wa raia na mali zao..”
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 2 Disemba 2025 wakati akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC Jijini Dar es Salaam.


