
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป amesema kwa namna moja au nyingine kuna baadhi ya taasisi za dini zimejiingiza kwenye mkumbo ambao unaendelea wenye nia ovu ndani yake.

Akieleza juu ya uongozi wa nchi katika kufuata misingi ya katiba na sheria, Rais Dkt. Samia amesema Tanzania haina dini lakini Watanzania wana dini za madhehebu mbalimbali huku akisisitiza kuwa kikatiba na sheria za nchi hakuna dini na dhehebu lolote lenye uwezo waโkuover rideโ madhehebu mengine.
Akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo tarehe 2 Disemba 2025, Rais DKt. Samia ameyasema na kuyasisitizia haya kuhusu taasisi za dini nchini
โViongozi wa dini msijivishe majoho ya kwamba nyinyi ndio mnaweza โkuover runโ nchi hii, hakuna. Tutakwenda kwa kwa Katiba na Sheria ya Nchi hii.โ

โHatutaendeshwa na madhehebu yoyote ya dini, madhehebu ya dini na wafuasi waoโ
โubora wa dini upo miyoyoni kwetu, wale wanaoamini ndio wanajua ubora wa dini yao..โ
โhakuna โover ridingโ hapa! Kwamba โmimi dini yangu ndio itaover ride Tanzania na tamko nikilitoa ndio hilo hiloโ.
โโฆhata wenyewe wanatofautiana, mimi toka nimekaa matamko 8 yametolewa na TEC, lakini ukienda chini chini wenyewe wanapingana, matamko yale hayafanyi kazi.. .waliosimama kwenye mstari wa haki wanaona ni batili iliyofanyika..hawaungani nao..โ
โTanzania yetu ni nchi ya umoja na mshikamano, amani na utulivu ndio ngazo zetu, tusivurugwe ndugu zangu..โ






