Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป, amesema Serikali anayoiongoza ya awamu ya sita si serikali ya kuamrishwa, kupewa masharti, au kuelekezwa namna ya kuendesha majadiliano na wadau mbalimbali wa mambo ya kisiasa.
Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linalojiongoza kwa misingi ya mamlaka yake kamili na si kundi la watu linaloweza kushinikizwa.
Akizungumza wakati wa mkutano wake na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam aliokutana nao leo tarehe 2 Disemba 2025 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC Jijini Dar es salaam, Rais Dkt alipokutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kituo cha mikutano cha kimataifa JNICC Jijini Dar es salaam, Amesema kumekuwapo na taarifa za baadhi ya makundi ya kisiasa na watu wanaoendelea kutoa masharti kabla ya kukubali kukaa meza moja kufanya mazungumzo, ikiwamo masharti ya โmfanye hiliโ, โmwachie huyuโ, au โtekelezeni kigezo hiki kabla ya kuzungumza.โ
“..wanadamu hukosana na wakaelewanaโฆinawezekana kabisa kuna mapungufu na hakuna serikali yoyote duniani isiyo na mapungufu lakini wanakaa, wanazungumza na kuondoa mapungufu yaliyopo.”
Kwa msisitizo, Rais Dkt. Samia โSerikali hii si ya kuamrishwa wala kupewa maelekezo,โ
Aidha, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa mazungumzo yanayokusudiwa ni yale ya kuheshimiana na kutambua nafasi ya kila upande.








