Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) imetumia uwezo wake wa kisheria kuiandikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuondoa mashtaka ya uhaini yaliyokuwa yakiwakabili Mfanyabiashara Jenifer Jovin (Niffer) na Mwanataaluma wa Habari, Mika Chavala.
Wakili wa Serikali Titus Aron aliieleza Mahakama kuwa, DPP hana tena nia ya kuendelea na mashitaka hayo – hatua iliyofungua njia kwa Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamua kuridhia ombi la Jamhuri na kuamuru kuwaachia huru washtakiwa.
Kumbukumbu zinaonesha wawili hao walikuwa wanakabiliwa na kesi namba 26388/2025 chini ya kifungu 92(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 20, toleo la marejeo ya 2023.



