Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media
Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara , Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora nahakikisha inaboresha Maendeleo ya Raslimali watu Nchini Kwa kuwekeza nguvu kuimarisha Elimu,kutoa Mfumo kazini na Usimamizi kwa Watumishi waliopo kazini na wanaingia kwenye Soko la Ajira
Amebainisha hayo jana Waziri Ofisi ya Rais -Menejmeti ya ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete ambapo amesema kuwa juhudi hizo zinaendana na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2015/2020 pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inayotilia mkazo kujenga uchumi unaotegemea maarifa.

“Serikali inaendelea kupanua wigo wa nafasi za ajira zinazolenga kuimarisha utoaji wa huduma za jamii, ambapo zaidi ya vibali 41,500 vilitolewa katika mwaka wa fedha 2015/2016, vikiwemo walimu wa masomo ya sayansi, hisabati na wataalamu wa afya” amesema Waziri.
Hata hivyo alibainisha kuwa upanuzi wa ajira hizo umelenga kuongeza idadi ya wataalamu waliobobea katika sekta muhimu za maendeleo.
Sambamba na hayo Waziri Amesema kuanzia Desemba 13, 2025, Serikali itaanza mchakato mpya wa uajiri ambao utazingatia zaidi uwezo, ujuzi na vipaji kupitia mtihani wa online aptitude test utakaofanyika katika vyuo vikuu, VETA na shule zenye maabara za kompyuta. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha vijana wanaingia kwenye ajira wakiwa na maandalizi ya kitaaluma na ujuzi stahiki
Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua, Waziri Ridhiwani alisema wizara yake inatekeleza wajibu wa kuhakikisha kuwa mfumo wa elimu ya watumishi na maendeleo ya taaluma unalindwa, unasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo.
Hata hivyo katika mkakati wa kuinua elimu ya umma, Ulizinduliwa mfumo wa Mrejesho (*15400#) utakaowezesha walimu, wanafunzi, wazazi na wadau wa elimu kutoa maoni, maombi na mapendekezo kuhusu huduma za elimu na utoaji wa taaluma kwani mfumo huo ni muhimu kwa kupata mrejesho wa moja kwa moja kuhusu changamoto katika sekta ya elimu.

”serikali imeanzisha Daftari la Huduma za Serikali (GSD) litakalowawezesha wananchi kupata kwa urahisi taarifa za huduma za elimu, taratibu za usajili, gharama, maeneo ya taasisi kwa njia za kuwasiliana na mamlaka husika”, ameeleza Waziri
Kuhusu changamoto za maadili miongoni mwa watumishi, kazini Waziri amesema marekebisho ya sheria za maadili yatawasilishwa bungeni ili kuimarisha uwajibikaji katika sekta ya elimu na kulinda heshima ya taaluma.
Licha ya changamoto za awali katika mifumo mipya, Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mageuzi ya rasilimali watu yanakwenda sambamba na mahitaji ya elimu ya kisasa na soko la ajira, kwa lengo la kuijenga Tanzania yenye wataalamu mahiri, wenye ushindani na uwezo wa kuleta maendeleo.
Aidha Wizara inatoa salamu za pole kwa familia ya Aliyekuwa Waziri wa Afya marehemu Jenista Mhagama, kwani alikuwa kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika kukuza utumishi wa umma na kuwa mfano wa kuigwa kwa watumishi wengi.

