Makamu wa Rais awasili Ruvuma kushiriki mazishi ya Jenista Mhagama
JamhuriComments Off on Makamu wa Rais awasili Ruvuma kushiriki mazishi ya Jenista Mhagama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea mkoani Ruvuma leo tarehe 15 Desemba 2025. Makamu wa Rais anatarajia kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama, yatakayofanyika katika Kijiji cha Ruanda mkoani Ruvuma tarehe 16 Desemba 2025.