Na Joseph Mahumi, WF, Arusha

Serikali imewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kuongeza ubunifu, uongozi bora na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ufanisi, uwazi na tija katika matumizi ya fedha za umma.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua Kongamano la 16 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lenye kaulimbiu ya “Kukuza Wataalam wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi watakaojiimarisha katika Ujuzi wa Uongozi na Ubunifu” lililoandaliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.

Mhe. Mhandisi Munde, alisema Serikali imejipanga kuimarisha usimamizi wa manunuzi kupitia Mfumo wa Kidigitali wa Ununuzi wa Umma, maarufu kama NeST, ili kupunguza gharama za ununuzi, kuongeza uwazi, kasi ya utekelezaji, kuzingatia bei ya soko, na kuleta tija kwa Taifa.

“Serikali imeelekeza shughuli zote za ununuzi zifanyike kupitia Mfumo wa NeST ili kuongeza uwazi, kupunguza gharama, na kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana katika miradi ya maendeleo,” alisema Mhe. Mhandisi Munde.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) CPSP. Godfred Mbanyi, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 16 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lenye kaulimbiu ya “Kukuza Wataalam wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi watakaojiimarisha katika Ujuzi wa Uongozi na Ubunifu” lililoandaliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.

Aliongeza kuwa, utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unategemea sana weledi na uadilifu wa wataalam wa ununuzi na ugavi, hivyo Serikali itahakikisha Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma zinazingatiwa kikamilifu katika ngazi zote za Serikali na sekta binafsi.

Aidha, Mhe. Mhandisi Munde aliiagiza PSPTB kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ili kuhakikisha shughuli zote za ununuzi na ugavi nchini zinafanywa na wataalam waliosajiliwa rasmi na PSPTB.

“Waajiri wote nchini wahakikishe wanawatumia wataalam waliosajiliwa na PSPTB kama inavyoelekezwa na Sheria Na. 23 ya Mwaka 2007 ilivyoanzisha PSPTB, hii italeta weledi, uwajibikaji na kuepusha upotevu wa fedha za umma,” alisisitiza Mhe. Mhandisi Munde.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mhandisi Munde, alisema kuwa Kongamano hilo ambalo limewaleta pamoja wataalam, wakufunzi na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kujadili namna ya kuimarisha ufanisi katika ununuzi na ugavi ni sehemu sahihi na imara kwa watalaam hao katika kujijenga, hivyo washiriki watumie fursa hiyo kupata maarifa mapya na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PSPTB, CSP. Jacob Kibona, alisema kuwa PSPTB imeendelea kusimamia na kukuza fani ya ununuzi na ugavi kwa uendelea kuhuisha mitaala ya mafunzo ya kitaaluma yenye kujikita katika umahiri ili kuzalisha wataalam wenye ujuzi na umahiri katika utendaji wa mnyororo wa ugavi, pia kuendesha mitihani ya kitaaluma na kutunuku vyeti vya kitaaluma katika ngazi ya stashahada, shahada, na cheti cha kitaaluma cha juu (Certified Procurement and Supply Professional).

Baadhi ya Wataalam wa Masuala ya Ununuzi na Ugavi wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la 16 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lenye kaulimbiu ya “Kukuza Wataalam wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi watakaojiimarisha katika Ujuzi wa Uongozi na Ubunifu” lililoandaliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.

“Utekelezaji huu umefanyika kupitia Miongozo ya Udhitibiti wa Mitaala (Curriculum Accreditation Guidelines) ili kulinda viwango vya taaaluma na kuleta usawa kwa wahitimu wa fani ya ununuzi na ugavi katika vyuo vyote nchini ikiwemo vyuo vya umma na binafsi” alisema CSP. Kibona.

Aliongeza kuwa PSPTB imeendelea na zoezi ya kusajili watalaam wa fani ya ununuzi na ugavi kwa mujibu wa sheria ya PSPTB ili kuendelea kuboresha kanzi data ya watalaamu hao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) CPSP. Godfred Mbanyi, aliwapongeza washiriki wote walioshiriki kongamano hilo kwa kuwa ni mfano bora katika maendeleo ya fani hiyo nchini.

Aliongeza kuwa PSPTB itaendela kutimiza vyema majukumu yake kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha fanyi inakuwa tija kwa taifa na usimamizi wa rasilimali za umma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) CPSP. Godfred Mbanyi, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 16 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lenye kaulimbiu ya “Kukuza Wataalam wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi watakaojiimarisha katika Ujuzi wa Uongozi na Ubunifu” lililoandaliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.