Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amefika nyumbani kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Leonard Qwihaya, Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam, kutoa pole kufuatia kifo cha mama mzazi wa Qwihaya Laurencia Shija Mabella.