Makumbusho ya Taifa ya Tanzania (NMT) imepokea zaidi ya watalii 100 walioingia nchini kupitia meli ya kifahari ya utalii (Cruise Ship), Ziara hiyo ni uthibitisho wa kuimarika kwa sekta ya utalii wa kitamaduni na juhudi za Serikali katika kufungua na kukuza masoko mapya ya utalii.

Watalii walitembelea vituo mbalimbali vya Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kujifunza historia, utamaduni na urithi wa Taifa la Tanzania.

Makumbusho ya Taifa la Tanzania inaendelea kujipanga kutoa huduma bora na zenye viwango vya kimataifa ili kukidhi ongezeko la watalii wanaotarajiwa kuendelea kuingia nchini katika msimu huu wa utalii.