Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema atatangaza hali ya dharura katika sekta ya nishati kote nchini humo.

Zelensky amesema hatua hiyo itawezesha kushughulikia operesheni za usambazaji wa umeme ziliovurugika kufuatia mashambulizi ya Urusi kwenye miundombinu ya nishati.

Kauli ya Zelensky imetolewa huku maafisa wa vikosi vya dharura wakiendelea na juhudi za kurejesha umeme mjini Kyiv ambako majengo karibu 300 ya ghorofa yalilengwa na shambulio la Urusi wiki iliyopita. Karibu kaya 6,000 hazina umeme kutokana na mashambulizi hayo.

Waziri mpya aliyeteliwa wa Nishati Denys Shmyhal amesifu maandalizi ya jiji la Kharkiv katika kipindi hiki cha baridi kali, na kutaja kuwa mji mkuu Kiev wenye wakazi karibu milioni 3 haukuwa umejiandaa vizuri, na ndiyo maana hatua za dharura ni lazima sasa zichukuliwe.