WATU 21 wamefariki dunia na wengine wapatao 30 wamejeruhiwa vibaya baada ya treni mbili kugongana kusini mwa Uhispania usiku wa Jumatatu (Januari 19).
Waziri wa Usafirishaji wa Uhispania, Óscar Puente, amesema treni hizo za mwendokasi yaligongana majira ya saa moja na dakika arubaini usiku karibu na mji wa Adamuz kwenye jimbo la Kordoba, Andalusia.
Shirika la reli la nchi hiyo, Renfe, linasema kwa ujumla watu 100 wamejeruhiwa, 30 kati yao wakiwa na hali mbaya sana.Huduma za usafiri baina ya mji mkuu, Madrid, na Andalusia zimesitishwa kwa muda.
Waziri Mkuu Pedro Sánchez ameuita usiku wa jana kuwa wa huzuni kwa taifa zima. Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ametuma sala (SW): Watu 21 wafa kwa… mu za rambirambi kwa waathirika wa ajali hiyo.


