Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema kuwa kama Urusi ingetaka kweli kumaliza vita, ingejikita katika diplomasia badala ya kujaribu kudhuru mitambo ya nyuklia ya Ukraine.

“Iwapo Warusi wangekuwa na nia ya dhati ya kumaliza vita, wangejikita kwenye diplomasia, siyo mashambulizi ya makombora, siyo kukata umeme, wala majaribio ya kudhuru hata mitambo yetu ya nyuklia,” Zelensky alisema katika hotuba yake.

“Tuna taarifa kuhusu maeneo ambayo Urusi ilifanya upelelezi kwa ajili ya mashambulizi. Kila kitu kinaonesha wazi kuwa diplomasia si kipaumbele kwa Urusi.

“Ni lazima tukiri hili. Ni muhimu kuendelea kuiwekea shinikizo nchi mvamizi, kwani chanzo halisi cha vita hivi kiko Moscow. Wiki hii tutafanya kazi kuhakikisha kuna shinikizo jipya na msimamo wa wazi wa dunia dhidi ya Urusi,” alisema.