Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi akizungumza na Wawakilishi wa Kampuni ya Condor, kutoka nchini Brazil, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na kudhibiti uhalifu, ambapo nchi mbili hizo, Tanzania na Brazil walibadilishana uzoefu katika masuala ya udhibiti wa uhalifu.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Meneja Mauzo ya Kimataifa kutoka Kampuni ya Condor,Renani Annize, Mkuu wa Mauzo ya Kimataifa, Kareem Seklawi na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Uwekezaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (TISEZA),James Maziku.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Makao Makuu ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (TISEZA), jijini Dar es Salaam.







