Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026, amezungumza katika Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 unaofanyika katika Ukumbi wa Mabeyo, jijini Dodoma.‎

‎Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na umewahusisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Lishe kutoka mikoa yote nchini.‎

‎Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Ndejembi amewasihi Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa miradi ya nishati inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kufanikisha azma ya Serikali ya kusogeza huduma bora za nishati kwa wananchi.