Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid akiwa na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Mhe. Ricardo Ambrosio Mtumbuida alipofika kuwasilisha salamu za pole katika Ofisi za Ubalozi wa Msumbiji jijini Dar es Salaam leo 22 Januari 2026, kufuatia maafuriko yaliyoikumba nchi hiyo na kusababisha takriban watu 600,000 kupoteza makazi.