Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Kusukuma na Kuhifadhi Maji katika mkoa wa Mwanza, mradi unaolenga kuboresha usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

“Miradi hii ni kwa ajili ya maendeleo yenu. Tunahitaji uwajibikaji na mshikamano. Watendaji wote wanapaswa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati,” — Dkt. Mwigulu Nchemba

Mradi huu unagharimu takribani Bilioni 46.2 na umekusudiwa kuwanufaisha zaidi ya wakazi 450,000 wa Jiji la Mwanza na Wilaya za Magu na Misungwi, ikiwemo maeneo kama Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyahingi, Luchelele, Sahwa, Kishiri, Igoma, Kisesa, Bujora, Kanyama, Fela na Usagara, kwa kuhakikisha huduma ya maji safi, salama na ya uhakika kwa kila mwananchi.