Theluji na mvua kubwa ambayo imenyesha kwa muda wa siku tatu zilizopita nchini Afghanistan, zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100 kote nchini humo.

Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Yousaf Hammad amesema watu 61 wamekufa na 110 wamejeruhiwa, wakati nyumba 458 zimeharibiwa kabisa au kwa sehemu na mamia ya wanyama wamekufa katika mikoa 15 kati ya 34 ya nchi hiyo.

Amesema idadi hiyo, inaweza kubadilika kadiri mamlaka inapoendelea kukusanya taarifa zaidi kutoka mikoani.

Afghanistan iko katika hatari kubwa ya kukabiliwa na matukio mabaya ya hali ya hewa, huku theluji na mvua kubwa ambayo husababisha mafuriko mara ikiwauawa makumi na wakati mwingine mamia ya watu kwa wakati mmoja.