Na Mwandishi wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam

Diwani wa kata ya Kigogo Manispaa ya Kinondoni Nasibu Limira amesema kuwa ndani ya siku 100 ya Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Sekta ya afya, elimu na miundombinu.

Akizungumzi na Waandishi wa habari Dar es salaam January 24,2026 katika mahojiano maalumu Diwani huyo amesema amebainisha kuwa Serikali inawapenda na kuwajali watu wa umri huo kwani ndiyo kundi ambalo hukumbwa na magonjwa mara kwa mara na wengine hawana uwezo wa kugharamia matibu.

“Kama rais Dkt.Samia alivyotoa ahadi yake ya siku mia moja,tayari tumeanza kuona baadhi ya mambo aliyoahidi yameanza kutekelezwa kwa kasi kubwa sana katika upande wa sekta ya Afya kwa Wazee kupatiwa uhakika wa matibabu bure .” Amesema Diwani.

Diwani Alamesema Hospitali ya Kigogo Licha ya kutoa huduma nzuri lakini wanakabiliwa na ufinyu wa eneo ambapo hawana eneo la kejenga jengo Kwa ajili ya kuhifadhia maiti kwani waliketewa mashine wakakosa eneo hivyo wameigwa katika hospitali nyingine za Serikali

Sambamba na changamoto hiyo watapeleka wazo katika Baraza la Madiwani wapewe fedha ili wawalipe Wananchi waliozunguka eneo la hospitali wahame ili wapate sehemu ya kujenga jengo la kuhifadhia maiti na wagonjwa.

Kwa upande wa elimu diwani amebainisha kuwa kuna baadhi ya shule ambazo hazijajengewa ukuta hivyo inahiyajika fedha za kuwalipa wananchi waliozunguka shule ili wahame hivyo katika uongozi wake atajitahidi anashirikiana na Serikali pamoja na Wadau wa maendeleo kutekeleza suala hilo

Aidha kuhusu ulinzi na usalama umezidi kuimarika watu wamekuwa wakiendelea shughu amesema kuwa wamekua wakisisitiza ulinzi shirikishi,nakutoa elimu kwa Wananchi kutambua umuhimu wa kuchangia ulinzi shirikishi.

Katika mitaa yetu mitano hali ni shwari,lakini bado tuna malengo na Ofisi ya Serikali iliyochomwa yunasubiria Serikali ilete fedha ili ukarabati ifanyike na wananchi waendelee kupatiwa huduma za kiofisi.