Na Mwandishi wetu,JamhuriMedia
Dar es salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Taifa Profesa Ibrahim Lipumba ametoa Wito kwa wanachama wa Chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla kuacha kubaguana kwa dhana ya udini, Uzanzibari na Utanganyika.

Profesa Lipumba amesema hayo Januari 27,2026 wakati wa dua ya kuwaombea wanachama wa chama hicho waliopoteza maisha kwenye maandamano ya kisiasa yaliyowahi kufanyikaa Januari 27, 2021 Pemba Visiwani Zanzibar ambapo watu takribani 71 walipoteza maisha na wengine Kuumia pamoja na kukimbia Uhamishoni Mombasa Kenya

Aidha amesema migogoro ya kisiasa imekua ikitokea na baada ya Uchaguzi wa Taifa madai ya kutangazwa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo hali hiyo isiwafanye Watanzania wabaguane kutokana na dini,Utanganyika na Uzanzibari

Tusikubali kugawanyika kidini,tusiingie kwenye mtafaruku wa aina yoyote,kwani Sisi ni Taifa moja kama kuna kutoelewana tunatakiwa kukaa meza moja kufanya mzungumzo au Maridhiano tusisababishe Damu za watu wasio na hatia kumwagika’ amesisitiza Prof

Nakuongeza “sisi CUF ni chama ambacho kinasimamia umoja wa Kitaifa,chama kinahakikisha Wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar wanapata haki sawa bila kuwepo ubaguzi wa aina yoyote”.

Aidha amewambia Wananchama wa CUF kuwapuuza wale wanaokuja na agenda ya kudai kuwa wanachukiwa kwasababu ni Wazanzibar,nakwamba migogoro yote ya isuluhishwe kwa amani.

Ameongeza kuwa Chama Cha CUF, kitaendelea kusimamia umoja, amani kwa Watanzania wote bila kujali utofauti wa dini na kisiasa na kuwataka Watanzania kukataa agenda ya kubaguana.

Amesisitiza kuwa matatizo katika nchi yanapotokea ni vyema yakatatuliwa kwa njia ya amani na utulivu ili kuendelea kujenga misingi ya amani na utulivu.

Ikumbukwe kuwa Januari 27 ya kila mwaka(CUF )inaadhimisha mauaji ya wanachama wa CUF waliouawa tarehe 26 na 27 katika maandamano wakidai uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2000 urejewe,katiba mpya ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tume huru ya uchaguzi,Utawala Bora wenye misingi ya kufuata Sheria