Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo tarehe 29 Januari 2026, ametembelea na kukagua ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Luthuli, Posta Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ambaye yupo Jijini Dar es Salaam kwa shughuli mbalimbali za kikazi amekagua maendeleo ya ukarabati pamoja na uwekaji wa vifaa na samani katika ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo.

Baada ya ukaguzi huo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi, amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba ukarabati huo umekamilika kwa asilimia mia moja na Jengo litakuwa tayari kwa matumizi kuanzia tarehe 04 Februari 2026.