Bodi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia, IAEA, itakutana leo kujadili usalama wa nyuklia nchini Ukraine.
Kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya Urusi, nchi 13 zikiongozwa na Uholanzi zimeiomba bodi hiyo ya IAEA kukutana kuhusiana na hali ilivyo sasa nchini Ukraine na athari zake za usalama wa nyuklia.
Katika barua iliyoandikwa Januari 21 iliyoonekana na AFP, wanachama wa shirika hilo walisema kuwa wajumbe wao wana wasiwasi kuhusu hali hiyo inayotokana na vita nchini humo.
Pia imesema mashambulizi ya hivi karibuni nchii Ukraine yamesababisha uharibifu mkubwa zaidi wa miundombinu ya nishati, ambayo inachukuliwa kuwa muhimu kwa uendeshaji salama wa vinu vya nyuklia.



