Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media
Dar es Salaam

Kata ya Mbezi iliyopo Halmashauri ya Ubungo Dar es Salaam katika siku 100 za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vivuko, barabara, Ukarabati wa shule 12 na kukamilika kwa Kituo Cha Afya Msakuzi.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo January 30,2016 Diwani Nyantori Pius ameshukuru jitihada za Rais kupitia serikali yake ndani ya siku 100 kwa kutoa fedha kiasi Cha Shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya vivuko na zaidi ya Shilingi Milioni 600 kukarabati shule 12 na zaidi ya Bilioni 19 ujenzi wa barabara ya Msumi ambayo inatakiwa kukamilika mwezi wa nne.

Ameongeza kuwa kazi inayofanywa Rais Samia kuwafikia wananchi wa choni inassidia katika kutatua kero wanazokumbana nazo ikiwemo ujenzi wa miundombinu hiyo ambayo itarahisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa urahisi ndani ya mitaa mitano ya Kata hiyo.

Kuhusu Kituo Cha Afya Diwani Nyantori amesema wameshakabidhiwa Zahanati ya Msakuzi ambayo tayari imeanza kufanya kazi sambamba na Kituo Cha Afya Cha Mpiji Magohe ambacho kimeboreshwa kutoka Zahanati Hadi ngazi ya Kituo Cha Afya.

Amesema Kata ya Mbezi imenufaika na miradi ya maji licha ya kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa maji kutokana na ukame unaoendelea ambapo pia Rais Samia ametoa zaidi ya Bilioni 1.9 kwa ajili ya mradi wa maji wa mtaa wa Msumi ambapo ujenzi wa mradi huo tayari umeshaanza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Louis Bawaziri Hassan Tandala amesema ndani ya siku 100 za Rais Samia wamefaidika na ujenzi wa daraja la Kasambala ambalo nyakati za mvua lilikuwa kikwazo kwa wananchi hususani wanafunzi kuvuka ambapo linagharimu zaidi ya Milioni 600.

Kuhusu sekta ya elimu amesema shule ya Msingi Mbezi umepewa zaidi ya Milioni 45 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya majengo Ili wanafunzi wasome katika Mazingira Bora huku wakipokea zaidi ya Milioni 47 kwa ajili ya kujenga Kituo Cha Walimu ambapo watakuwa wanakutania kujadili mambo yao.

Licha ya mafanikio hayo amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya wingi wa wanafunzi ndani ya shule moja pamoja na ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya mtaa huo licha ya uwepo wa mifumo ya maji kwa asilimia 99.