Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange amehimiza wananchi kuyatumia madampo kukusanyia taka ili zitumike kama malighafi pamoja na kusafisha mazingira.

Ametoa wito huo wakati wa ziara ya kukagua shughuli za uchakati wa taka katika Kiwanda cha kuzalisha mboji Mabwepande Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Februari 23, 2026.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Dugange ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kukaa pamoja na kuja na mkakati wa kuhamasisha wananchi kutumia kiwanda hicho kwa kukusanya takaoza na kuzipeleka ili zichatwe kuwa mbolea.

Halikadhalika, kutokana na kuwa asilimia 60 ya taka ni zinazozalishwa na kutupwa katika madampo ni zile zinazooza, aliwahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kuzikusanya kwa ajili ya viwanda vya mbolea ya asili.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazungira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akiwasili katika kiwanda cha kuzalisha mbolea Mabwepande wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Februari 23, 2026 kwa ajili ya kukagua shughuli za uchakati wa taka.

“Kiwanda hiki ni kikubwa kwa Dar es Salaam na nchi nzima nikuonbe DC (Mkuu wa Wilaya), Mkugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na Menejimenti mkae na muandae mkakati kuona namna gani mnaweza kuvutia wananchi waone taka ni fursa na kuzileta hapa,” alisema.

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itakuwa bega kwa bega na kushauri pale inapobidi nini cha kufanya ili kuhakikisha kiwanda kinafanya vizuri zaidi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Dugange alitembelea dampo la Pugu Kinyamwezi

Aidha, Dkt. Dugange alielekeza Baraza la Taifa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutumia sheria kudhibiti taka za platiki.

Alisema taka za plastiki katika madampo zimekuwa nyingi hali inayonesha pamoja na kupigwa marufuku uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mkfuko hiyo bado inaonekana kutumika.

Vilevile aliuhimiza uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea kufuatila kwa karibu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata takaozo ili zitumike katika uzalishaji wa mbolea.

Naibu Waziri alitumia nafasi hiyo kuwashauri kutumia madampo kusajili
Akiwa katika ziara hiyo Dkt. Dugange amesema mradi huo unasaidia katika udhibiti wa taka oza kutoka masoko na maeneo mbalimbali ya jiji.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha Mabwepande Mhandisi Jimson Mkenda alisema mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa ufadhili wa Jiji la Hamburg, Ujerumani kwa Serikali ya Tanzania wa Euro 2,506,277 sawa na shilingi 6,339,276,792.72 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na uendeshaji.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazungira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za uchakati wa taka na kuzalisha mbolea katika mradi wa kiwanda cha Mabwepande wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Februari 23, 2026. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni Mhe. Saad Mtambule.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazungira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akiwa katika zaiara ya kutembela na kukagua dampo la Pugu Kinyamwezi wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam leo Februari 23, 2026.