Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imesaini makubaliano Maalum na Benki ya CRDB yatakayorahisisha upatikanaji wa huduma za fedha kwa wachimbaji wadogo wa madini.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde
amesema katika hatua hiyo ni ya kwanza kihistoria kwa Kikundi cha Wachimbaji Wadogo cha Songwe Gold Family kupata mkopo wa sh. bilioni 50 kwa wakati mmoja kutoka benki ya CRDB.
Mavunde amesema jambo hilo, halijawahi kutokea nchini,benki ya CRDB pekee ndiyo iliyofanya uthubutu wa jambo hilo kwa wachimbaji wadogo.
Waziri mavunde amesifu hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi za makusudiza serikali kujenga mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa kuimarisha uchimbaji.
“Tunawapongeza CRDB kwa kwenda “field”, kujionea uhalisia wa shughuli za uchimbaji, na kufanya maamuzi kupata taarifa sahihi na siozilizopikwa’’amesema.
Aidha katika hatua nyingine amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa utashi na uongozi thabiti unaoendelea kuibadilisha Sekta ya Madini kuendelea kuwavutia wawekezaji .
Amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanzisha Mfuko wa Dhamana kwa ajili ya kukopesha wachimbaji wadogo, ili kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa mitaji na kuongeza kasi ya urasimishaji wa shughuli za uchimbaji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, amempongeza Waziri Mavunde kwa kuhakikisha mageuzi haya yanafikiwa katika kipindi cha uongozi wake
Kwa kushawishi Taasisi za Fedha, kuwekeza katika Sekta ya Madini na leo ni ishara ya mafanikio ya jitihada hizo.
Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema mpango huo ni wa kihistoria kwa benki kwenye Sekta ya Madini, kwani unaweka mfumo wa kisasa na shirikishi unaoendana na uhalisia wa wachimbaji wadogo.
Kwa kuwa wanabeba sehemu kubwa ya sekta inayokua kwa kasi ,kwa miaka
mitano mfululizo kuliko sekta nyingine.
Dkt. Nsekela,amesema mpaka sasa tayari CRDB imeshatoa T,sh bilioni 186 kwa Sekta ya Madini, kati ya hizo bilioni 136 kwa wachimbaji wakubwa na bilioni 50 kwa wachimbaji wadogo.
Aidha amesema tofauti kubwa ya mpango huo ni aina ya dhamana, si azima kutumia mali zisizohamishika, dhamana zitajumuisha leseni halali za uchimbaji, leseni ya biashara ya dhahabu, hifadhi ya dhahabu ya mkopaji, pamoja na mikataba maalum.
“CRDB iliziona changamoto kwa wachimbaji ni ukosefu wa mitaji, teknolojia, na ushauri wa kitaalamu kwa hiyo huu ni mpango wa mkakati wa kitaifa unaojumuisha elimu ya kifedha, urasimishaji wa shughuli, na
kuimarisha mchango wa sekta”amesema.
Kwa upande wa wachimbaji wadogo, Rais wa FEMATA, John Bina, amesema
wachimbaji watakwenda kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kulifanikisha jambo hilo .
Amesema mpango huo ulikuwa kilio cha muda mrefu cha wachimbaji wadogo
na sasa unafungua ukurasa mpya wa maendeleo kwa sekta hiyo













