TAKUKURU Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kudhibiti fedha kiasi cha Shilingi Millioni 85,006,000 fedha ambayo ni madai ya walimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya jiji la Mwanza, madai ambayo yalicheleweshwa kwa zaidi ya miezi sita.

Mafanikio haya ni baada ya TAKUKURU kufanya Uchambuzi wa mfumo na Halmashauri kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na TAKUKURU ambapo imepelekea walimu hao 77 kulipwa stahiki zao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Abnery Mganga alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma.