Na Hassan Kimweri, WAF – Morogoro

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwa kuepuka uchafuzi wa mazingira, kuwa na matumizi sahihi ya maji safi na salama na unawaji wa mikono.

Dkt. Magembe ametoa rai hiyo leo Februari 25, 2026 kufuatia tamko alilolitoa leo la mwenendo wa magonjwa ya mlipuko na kumalizika kwa ugonjwa wa kipindipindu nchini ambapo takriban mwezi mmoja uliopita, hakujatokea kwa mgonjwa wa ugonjwa huo.

“Serikali imejipanga kufuatilia na kutoa huduma dhidi ya magonjwa yote ya mlipuko na itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara iwapo kutakuwa na mabadiliko katika mwenendo wa maambukizi au endapo kutahitajika kuchukua hatua zaidi,” amesema Dkt. Magembe.