Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, amekagua na kuridhishwa na Maendeleo ya matengenezo ya barabara ya Dodoma – Iringa eneo la Fufu ambalo lilikuwa likijaa maji kipindi cha mvua na kusababisha adha kwa wananchi wa eneo hilo. 

Waziri Ulega amekagua eneo hilo leo tarehe 25 Februari 2026 akiwa njiani kuelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ambapo amempongeza Meneja wa TANROADS mkoani Dodoma Mhandisi Zuhura Amani kwa kukamilisha mradi huo sambamba na uwekaji wa taa 46. 

Aidha Waziri Ulega amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa makalavati eneo la Manzase na uinuaji wa tuta ili kuondoa changamoto ya kujaa kwa Maji katika eneo hilo hasa kipindi cha mvua.