Na Baltazar Mashaka, JamhuriMedia, Mwanza

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ali, amewataka Waislamu nchini kuweka mikakati madhubuti ya kuleta maendeleo, kuimarisha mshikamano na kudhibiti mifarakano ndani ya jamii ili kulinda umoja na ustawi wa taifa.

Mufti aliyasema hayo leo, jijini Mwanza alipozindua kanzidata ya madrasa nchini, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu (BOT), Capripoint, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.

Mufti Zubeir alisema kuna umuhimu Waislamu kuwekeza katika elimu ya dini kwa watoto wao sambamba na elimu ya mazingira, uchumi na maadili ili kuwajengea msingi imara wa maisha na kupata kizazi chenye uwezo wa kulisaidia taifa siku za usoni.

“Ni wajibu wetu kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu sahihi ya dini na mazingira.Kupitia madarsa wanajengewa maadili mema na kuandaliwa kuwa rasilimali watu watakaosaidia maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza;

“Tusipowasomesha watoto htutapata watu wa kutusaidia.Tuangalie mbele kwa kizazi cha sasa, vijana tufanyeje wasiingie kwenye mmomonyoko wa maadili, tutafute ufumbuzi kama waislamu tunawafundishaje vijana wetu.Tukiwapa elimu, maadili na uchumi tutakuwa tumelisaidia taifa letu.”

Aidha, alieleza kuwa mshikamano miongoni mwa Waislamu ni nguzo muhimu katika kuimarisha taasisi za dini na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi,alionya dhidi ya migogoro na migawanyiko isiyo ya lazima inayoweza kudhoofisha juhudi za maendeleo.

“Kufarakana Waislamu ni jambo baya, n haramu na haifai kugombana taassisi na jumuiya zote, tutengeneze jambo moja, haya maendeleo tunayoyaona tukifarakana hayawezi kupatikana.Waislamu tukamate ardhi tutengeneze Tanzania yetu, serikali iko wazi na haya hamshughuliki nayo mtayakumbuka baadaye,” alisema Mutfi Zubeir.

Akizungumzia uzinduzi wa kanzidata hiyo , alisema kuwa, unatarajiwa kusaidia kuweka mfumo rasmi wa usajili na utambuzi wa madrasa nchini, hatua itakayorahisisha uratibu wwa walimu, upangaji wa mitaala na ufuatiliaji wa maendeleo ya taasisi hizo za kidini.

Kwa mujibu wa Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaj Hasan Kabeke, ni hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya elimu ya dini ya Kiislamu nchini, hivyo matarajio ya kanzidata hiyo itasaidia kuongeza uwazi, usimamizi na ubora wa elimu inayotolewa katika madrasa mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Katibu wa Mufti, Sheikh Mussa Hemed bin Hemed, alisema kuanzshwa kwa kanzadata ni maagizo ya Mutfi, lengo ni kuwa na taarifa za walimu wa madrasa katka ngazi zote, hivyo watasimamia kwa dhati kwa kuanzsha kurugenzi ya kusimama uendeshaj wa kanzidata hiyo.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, kabla ya kumkarbisha Mufti alisema, kuzinduliwa kwa ofisi za BAKWATA na Kanzidata mkoan humu, kazi hiyo ni kubwa kwa wanaoona mbalimbali na shughuli za madrasa lazima kuwe na ufuatiliaji, tathmini baada ya kuzitambua na kuzisajili.

“Madrasa ni sehemu ya maadili ya dini, pili kupata udhamini wa masomo nje ya nchi, kwa walimu wa madrasa, kusoma na kupata cheti cha utambulisho ndani na nje, ni jambo kubwa na mabadiliko makubwa ndani ya BAKWATA, hivyo kauli mbiu ya Mutfi, ‘Badilika, Jitambue Acha Mazoea’ inafanyika kwa vitendo,”alisema Mtanda.