Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambayo imebeba waombolezaji na jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi, ikiwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Iringa leo Machi 29, 2026.
Mwili huo umesafirishwa kutoka Dar es Salaam leo baada ya shughuli ya kuaga iliyofanyika jana Machi 28, 2026 katika Viwanja vya Karimjee.