Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia, Kibaha
WAKATI bei ya mafuta ikipanda zaidi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), umewasihi wasafirishaji na wamiliki wa vyombo vya usafiri kutopandisha nauli.
Mbali ya kuwasihi hivyo, mamlaka hiyo imelazimika kuitisha kikao cha dharura na wamiliki vyombo vya usarishaji kukutana Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana suala hilo zito.
Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Dk. Habib Suluo amewaambia waandishi wa habari mjini Kibaha mkoani Pwani Leo Aprili mosi, 2026 kuwa amechukuwa uamuzi wa kuitisha mkutano wa wadau wa ussafirishaji kutokana na bei ya mafuta kupanda zaidi, jambo ambalo linaweza kuathiri mwananchi wa kawaida.
“Kila mmoja wetu ni shuhuda katika hili bei ya mafuta imepanda, mamlaka tumeona ni vema wiki ijayo tukakutana na wamiliki na wasafirishaji kwa ajili ya kujadiliana suala hili…kupanda kwa bei ya mafuta kunagusa maisha ya watu mmoja mmoja.
“Nimewaiteni tuongee kidogo kwa mambo ambayo yametokea leo Aprili mosi,2026, tukio la kupanda kwa bei ya mafutam Dar es Salaam bei imefika 3820, ukienda mikoani imepanda zaidi hadi shilingi 4,000.

Mnafahamu sisi sote ni watumiaji wa usafiri huu ardhi ukiwamo mabasi ya mijini daldada nay ale ya mikoani na nchi jirani.
“Kutokana na halii hii mdhibiti ambaye ni mamlaka ana jukumu la kutoa mwongozo na kuwatak wasafirishaji wawe watulivu, suala hili tumeliona, tunafahamu vita vinavyoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran ndiyo sabbau kubwa ya kupanda kwa bei ya mafuta. Haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu bei kupanda hivi. Siku zote bei ya mafuta hutolewa na EWURA,”amesema.
Amesema kupanda kwa bei hiyo kunaweza kuathiri utoaji huduma mijini na vijijini na hata wasafirishaji wa mizigo kwa sababu kuna magari ya kodi ambayo kila siku lazima yasafiri.
“Kwa hiyo ili tuweze kwenda pamoja na kwa namna yoyote ile nauli zinapopanda anayeumia ni mlaji, LATRA jukumu lake kubwa ni kuhakikisha mtoa huduma anaendelea kutoa huduma na zinakuwa endelevu na mtoa huduma anaifikia huduma ile. Kwa vyovyote vile jambo kubwa ni kuhakikisha tunachukua hatua za haraka ikiwezekana ndani ya kipindi kifupi tuitishe kikao cha wadau ili tuyazungumze haya.
“Mamlaka ilitegemea kupanda kwa bei hii, japo kiwango kilichopanda ni kikubwa kiasi kwamba kuna watu wameanza kupandisha nauli bila kuzingatia taratibu, tunafahamu biashara yoyote kitu kikibadilika ghafla, haina maana siku hiyo hiyo unaanza kupata hasara. Kwa msingi huu tunaitisha kikao cha wadau kitakachofanayika Aprili 8, mwaka huu siku ya Jumatano.

“Nawaomba sana wasarishaji wawaone huruma Watanzania, hawa Watanzania vinapato vya vidogo hivi ndiyo vinawachangia kwenye uwekezaji wao, kwa namna yoyote ile tusitumie hii kama nafasi ya kuwaumiza…hata kwa imani zetu ni dhambi kutumia shida za watu kujipatia kipato, hata Mungu anaweza asikupatie Baraka kwenye biashara yao.
Katika kipindi hiki cha mpito tunawasihi sana msipandishe nauli bila idhini ya mamlaka na sisi hatutasita kuchukua hatua kali kwa sabbau umekwenda kinyume na sheria, tunaomba sasa tukae hatua migogoro tunazungumza, tukae mezani tuzungumze maana hatujui mwezi ujao hali itakuwaje… hili ni janga la dunia sasa hivi,”amesema
“Kikao hiki kitakuwa live ili hata wale ambao hawatakuja Dar es Salaam waweze kufuatilia kwenye mitandao ya kijamii na wanaweza kutoa maoni yao.Sheria inatutaka sisi tupande nauli na baada ya kufanya hivyo nauli inaidhinishwa na bodi ya wakurugenzi, inatangazwa kwenye gazeti la serikali, kisha kuanza kutumika ndani ya siku 14.
“Nimeona tukiitisha kikao kesho, kwanz watu watakuwa hawajajianda akuhudhuria,tunatoa siku saba, kinachopaswa kufanyika ni nini? Kanuni zetu za kupanga nauli ya 9(2) inataka mtoa huduma alete maombi LATRA endapo katika kipindi kisichopungua miaka mitatu mrejesho wa mtaji wake ni chini ya asiliamia 10.
Waje waonyeshe kwamba kwa bei hii ya kupanda mafuta mtejesho wetu wa mtaji tuliowekeza uko chini ya asilimia 10 kwa sasa, wanataka waje wathibitishie mamlaka.
“Tutawapa nafasi ya kufanya wasilisho alafu tutasikiliza watumiaji na wadau wengine, lakini bila kuathiri kanuni ya 9(2), Kanuni ya 9(3), inasema endapo ule mtaji au mrejesho wa mtaji utakuwa chini ya asilimia 10, ikawa chini ya miaka mitatu kwa sababu nauli zinazotumika sasa tulitangaza Desemba 8, 2023 maana yake miaka mitatu haijatimia.

“Mtoa huduma aje na hesabu zake atuambie kwa hesabu zangu nilizopiga na mrejesho wangu wa uwekezaji wa basi hili ni chini ya asilimia 10, upangaji wetu wa nauli ndivyo unavyotaka.
Mamlaka pia inalo jukumu chini ya kanuni ya 13 (1) kupanga tozo katika mazingira ambayo yanaweza kutokea kama haya, hata kama watoa huduma hawataleta maombi sisi tutatumia taarifa zetu tulizonazo.
Lazima tushirikiane na wenzetu wa EWURA maana hatujui hali hii itaendelea mpaka lini.
“Tusisahau wanaotakaiwa kubeba mzigo huu ni Watanzaniam sasa wao wamepata wapi hiyo nyongeza alafu mtoa huduma aendelee kupata shida, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kushindwa kwenda shule, tuiangalie hali ya Watanzania ilivyo sasa hivyi.
“Hata wasafirishaji watakapoleta maombi yao wazingatie haya, mambo muhimu ya kuwasilisha maombi wanatakiwa kuwa na leseni hai za mamlaka hiyo, kupeleka nauli inayopendekezwa, watoe sababu za kutaka nauli ipande, faida gani itapatikana kwa watumiaji, wapelekee kikokoto cha hesabu zao,wamiliki wanatakiwa kupeleka hesabu zao zote zilizokaguliwa,”amesema.
Amesema kati ya wasafirishaji wengi, wachache wanatunza hesabu zao za miaka mitatu mfululizo bila kuwa na shida yoyote.





