*Kukimbizwa kwa siku 195 Nchini
*Kufikia tamati Oktoba 14, 2026
*Hamasa kila Kona ya Pemba Kusini

Na Byarugaba Innocent, ORMV, Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi leo Aprili 2, 2026 amezindua Mwenge wa Uhuru na kutoa baraka za kukimbizwa kwenye Halmashauri Mikoa 31, Halmashauri 195 nchini ukiongozwa Wazo Michael Mwang’onda ambapo Mwenge wa Uhuru utatembelea, kukagua,Kuzindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi mbalimbali ya Maendeleo ukijikita kwenye kutazama thamani ya fedha zilizotumika na ubora wa Miradi iliyotekelezwa.

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika kwenye viwanja vya Gombani vilivyopo Wilaya ya Chakechake Mkoani Kusini Pemba ukishuhudiwa na maelfu ya Wananchi wakiwemo Wahe. Mawaziri, Wakuu wa Mikoa,Makatibu wa Wizara,Makatibu tawala wa Mikoa Wahe. Wabunge,wakuu wa Wilaya na Makatibu tawala, Vyama vya siasa pamoja na Wakuu wa Mashirika na taasisi zilipo nchini.

Makamu wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
amewashuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuifanya
Kusini Pemba kuwa Mwenyeji wa uzinduzi huo na Rais wa Zanzibar kuridhia kuwa Mgeni rasmi wa hafla hii muhimu ya uzinduzi

Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Mawaziri wenye dhamana ya uratibu wa Mwenge Mhe.Joel Arthur Nanauka,Waziri wa Nchi Ofisi Rais Maendeleo ya Vijana Tanzania Bara na Mhe.Shaaban Ali Othuman,Waziri wa Vijana, Ajira na uwezeshaji Zanzibar, Makatibu Wakuu na Kamati ya maandalizi kwa maandazili Mazuri.

Aidha,Mhe Mwinyi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kudumisha Amani, Umoja wa kitaifa na kudumisha Muungano wetu.

Kauli mbinu ya Mwenge wa Uhuru,2026 inasema Tanzania ni yetu sote,tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo