Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Jumanne Murilo amesema kwa sasa hali ya kiusalama ni shwali kutokana na jitihada za jeshi hilo

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Aprili 27, 2026, amesema hali ya usalama katika Jiji la Dar es Salaam ni shwari tofauti na siku za juma kutokana na ushirikiano kati ya Polisi na wananchi.

Murilo amesema kwa sasa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam ,inaendelea kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu kupitia taarifa zinazotolewa na wananchi na wadau wengine wa usalama.

Amesema Jeshi la Polisi tarehe 20/04/2026 eneo la Ubungo Dar es Salaam limewakamata watu 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao ikiwemo kutoa vitisho na lugha za matusi mazito kwa watu mbalimbali.

‘’Katika kundi hilo baadhi yao wamebainika ni wafanyakazi wa kampuni ya INNOVIX CALL CO LTD na OTAIGO FINANCIAL SERVICES COMPANY LIMITED inayojishughulisha na ukopeshaji wa pesa kwa njia ya mtandao.

Watuhumiwa hao ni Renatus Mujwahuzi @migeyo Mkazi wa Mbezi Beach, Odilia Oswin @ngunga Mkazi wa Goba njia nne, Theresia Brastius @kanu mkazi wa Mtoni Kijichi na wenzao 34.

Hatua zaidi zinachukuliwa ili kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria’’amesema

Amedai katika kutekeleza na kusimamia mifumo ya haki jinai Polisi Dar es Salaam, inawashukuru wananchi na wadau wengine wa usalama kwa kuendeleakuwashughulikia watuhumiwa wa vitendo vya kijinai kwa kutumia mifumo ya kisheria.

Aidha Polisi Dar es Salaam ina baadhi ya takwimu za kipindi cha mwezi Machi hadi Aprili 2026 ambazo baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na kufukishwa kwenye mifumo mingine ya kisheria.

‘’Walipatikana na hatia ni pamoja Hashimu Kasimu @duma mkazi wa Kimara
,alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti.

Vicent Laurent @ndimbo mkazi wa Urafiki Kinondoni alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka

Habibu Nassoro mkazi Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya
Temeke, kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti,Ismail Ally @muro Mkazi wa Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

Nelson Julius mkazi wa Mavurunza Kimara alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo, kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang ‘anyi wa kutumia silaha .

Fadhili Issa mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke ,kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka 7,Peniel Jonathan @mtakibaleza mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

Yusuph Iddi mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke ,kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi’’amesema.

Kamanda Murilo ameyoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na J.eshi la Polisi, kutoa taarifa mbalimbali zenye viashiria vya kihalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na kwenda mahakamani kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka.