Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali, Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuph Makamba katika makazi yake Tegeta Jijini Dar es Salaam.