Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepokea taarifa ya utekelezaji wa miongozo na taratibu za uratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kutoka kwenye Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana yenye dhamana na uratibu inayoongozwa na Joel Arthur Nanauka
Akiwasilisha pongezi hizo leo Oktoba 19, 2026 kwa niaba ya Kamati, Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Rejina Malima (Mb) amesema kamati imeridhishwa sana na maandalizi mazuri, makubwa yaliyofanywa na Wizara Kuanzia kwenye uzinduzi uliofanyika tarehe 2 Aprili,2026 kwenye viwanja vya Gombani Kusini-Pemba mpaka kilele kilichofanyika Manispaa ya Sumbawanga mkoani- Rukwa kwenye viwanja vya Nelson Mandela tarehe 14 Oktoba,2026
Aidha, Dkt.Malima ameongeza kuwa Kamati inampongeza Nanauka kwa hotuba nzuri aliyoitoa kwenye kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,2026 kuwa inasadifu timu nzuri aliyonayo kuwa inamsaidia vema katika kutekeleza majukumu ya Wizara kufikia Malengo ya utoaji huduma kwa Wananchi
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joel Arthur Nanauka ameishukuru Kamati hiyo kwa Michango, ushauri, Maelekezo na maboresho ambayo wamekuwa wakiyatoa mara zote kwani yamekuwa chachu ya kuwaimarisha zaidi na kutekeleza kwa tija na kuahidi kuendelea kuwa karibu ili kufikia mafanikio Bora zaidi.
Dkt.Kedmon Elisha Mapana akisoma taarifa ya utekelezaji kwa niaba ya Waziri Nanauka amesema kuwa Mwenge wa Uhuru 2026 ulikuwa na ujumbe unaobeba falsafa,Misingi,maadili na dhamira ya Kudumu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao unabaki kuwa sehemu ya ujumbe Mkuu.
Aidha,Dkt.Mapana ameongeza kuwa lengo la ujumbe wa Kudumu ni kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii ya Watanzania kuhusu;lishe Bora na afya imara, mafunzo ya Ufundi stadi, upimaji na ushauri wa afya,Mapambano dhidi ya rushwa,kuzuia Dawa za kulevya, Mapambano dhidi ya Malaria na kukuza Uzalendo na Mwenge.
Tarehe 2 Aprili,2026 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye viwanja vya Gombani Mkoa wa Kusini-Pemba alizindua rasmi Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na tarehe 14 Oktoba,2026 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Deogratius John Pancras Ndejembi amekuwa Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan baada ya kukimbizwa kwenye mikoa 31, Halmashauri 195 ukisafiri umbali wa kilomita 24,876.74 na kupitia miradi 1,337 yenye thamani ya shilingi 2,235,521,449,033.68.
Ikichagizwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ni yetu sote, tushikamane kuleta Maendeleo”




