Mwenyekiti mteule wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Dkt. Seif Rashid, amesema bodi hiyo imejipanga kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuunga mkono juhudi za mamlaka hiyo kufikia daraja la nne la ukomavu wa mifumo ya udhibiti wa dawa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza Oktoba 19, 2026, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, Dkt.Seif Rashid amesema yeye na wajumbe wenzake wanatambua ukubwa wa dhamana waliyopewa na wamejipanga kuitekeleza kwa weledi na uwajibikaji.


“Tumelipokea jukumu hili mimi na wenzangu. Viatu ulivyotupa ni vikubwa, lakini tutavivaa, na tunaahidi kufikia daraja la nne la ukomavu kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Afya Duniani,” amesema Dkt. Rashid.

Hata hivyo amesisitiza kuwa dhamira hiyo inalenga kuimarisha mifumo ya udhibiti wa dawa na bidhaa za afya, kuongeza ufanisi wa utendaji wa TMDA na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa za afya zinazokidhi viwango vya ubora na usalama Kwa mujibu wa viwango vilivyiwekwa na shirika la Afya duniani (WHO).


Kuzinduliwa kwa Bodi hiyo inatarajiwa kutoa mwelekeo wa kimkakati utakaoiwezesha TMDA kuimarisha utendaji wake, kuziba mapungufu ya udhibiti na kuweka msingi wa kufikia daraja la nne la ukomavu kwa mujibu wa viwango vya WHO