Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani
Baadhi ya wananchi Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani, wametaka serikali kuchukua hatua dhidi ya miradi ya maendeleo kwa kusuasua, ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara Tamco- Mapinga, wakieleza kuwa ucheleweshaji huo unarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ameeleza miongoni mwa miradi inayotajwa ni ujenzi wa barabara ya Tamco–Mapinga inayounganisha Wilaya za Kibaha na Bagamoyo, pamoja na mradi wa maji wa Pangani unaotarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya 70,000.
Mbunge jimbo la Kibaha mjini ,Silvestry Koka amesema hali ya miradi hiyo kutokamilika kwa wakati imekuwa inakatisha tamaa wananchi huku akiiomba serikali kukamilisha mradi wa barabara Tamco-Mapinga km 23 pamoja na mradi mkubwa wa maji kata ya Pangani.
Akijibu kuhusiana na miundombinu ya barabara ya Tamco-Mapinga meneja Tanroads Joel Mwambungu ameeleza kuwa, kilichokuwa kinakwamisha na mchakato wa malipo ya fidia kwa kipande cha km 12 ambapo kwasasa wahusika wameshalipwa.
Mkandarasi Kings Builders Mhandisi John Yongele Samson , ameeleza barabara hiyo ina urefu wa km 23 , ambapo awamu ya kwanza ilishatekelezwa kwa km 7 na awamu ya pili ni kipande cha km 14 kati ya hizo km 2 kimekamilika,.
Ameeleza wamechelewa kukamilisha mradi kwa kusubiria malipo ya fidia kwa wanaopisha mradi km 12 , sasa wanatarajia kuendelea na ujenzi hivyo wameshaandika maombi Tanroads kuomba mkataba mpya wa kuongezewa muda ambapo bado hawajajibiwa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo ameiagiza Tanroads kubadili mkataba ili mkandarasi aongezewe muda wa kimkataba ili mradi uanze.
Nyongo amefafanua barabara hiyo ni muhimu kufungua fursa za kiuchumi Kibaha na Bagamoyo hivyo amemuagiza meneja Tanroads kufika na taarifa ofisini kwake jumatatu oktoba 26,2026.






