Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.), tarehe 22 Oktoba 2026, amewasilisha taarifa za utekelezaji wa Wizara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Najma Giga (Mb.), jijini Dodoma.
Taarifa hizo zimejumuisha utendaji wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA), Monduli, Arusha, pamoja na utekelezaji wa mafunzo ya JKT kwa vijana wa kujitolea na wa mujibu wa sheria, kwa lengo la kutathmini mafanikio na kubaini changamoto zinazohitaji ufumbuzi.
Dkt Rhimo Nyansaho aliambatana na viongozi waandamizi wa Wizara, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.












