Na Aziza Nangwa,JamhuriMedia, Dar

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amewataka wadau wa utoaji maoni juu ya upandishwaji nauli za treni, lazima wazingatie maslahi ya pande zote mbili.

Lubigija amesema wadau katika mchakato wa utoaji maoni ,lazima wabebe jukumu la uwakilishi wa wenzao kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili.

Amesema suala la utoaji wa maoni juu ya kupandashwaji wa bei za treni ,kwenda,Kigoma,Mwanza na Arusha liko kisheria hivyo wadau wanatakiwa kulijadili kwa utulivu kwa kuzingtia maslahi ya umma.

“Hii ni fursa ya kuangalia namna gani iwe kwa mtoa huduma na mlaji pengine mtoaji anataka nauli ziongezwe kwa maslahi yake”amesema.

Amesema wananchi nao wana haki ya kuangalia tozo zinaendana na hali zao, kwa hiyo hakikisheni zinakuwa na maslahi kwa pande zote.

“Pengine mtoa huduma kama hakufanya maboresho anaweza kushindwa kutoa, huduma au mlaji anaweza kushindwa kulipia gharama hizo kutokana na hali yake”amesema.

Ameongeza kuwa Serikali inazingatia maslahi ya wananchi kwa kuangalia suala zima la utawala bora na ushirikishwaji, kwa hiyo inatakiwa utulivu na umakini katika kufikia maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya wote.

“Nafasi ya utoaji maoni kwa sasa ni kwa watu wa Dar es Salaam kwa hiyo ni vyema wananchi wakajitokeza na kushiriki kwa wingi kutoa maoni yao hata kwa kutumia webu site za LATRA au barua pepe kwa namna yanavyotaka”amesema.

Pia amewaomba wananchi kulinda na kuitunza, miundombinu ya Reli kwa maslahi ya taifa popote inapopita .

“Nampongeza Rais kwa kujenga miundo mbinu mizuri kwa usafiri wa Reli na anapenda mtindo wa ushirikishwaji kwa wananchi katika masuala yanayohusu maslahi ya taifa ili kuimarisha utawala bora kwa maslaahi ya umma”amesema.

Amesema amewapongeza sana LATRA kwa kuwa wasimamizi wazuri katika sekta wanayoisimamia, kwa hiyo wananchi wajitokeze kutoa maoni yao kwani wao wapo kama wasimamizi wa pande zote mbili.

Mkurugenzi wa wa Mamlaka ya Uzidhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habibu Suluo amesema amepokea maoni ya Shirika la Reli (TRC), kuhusu kuongeza nauli zake kwa treni ameyaleta mezani wadau waweze kujadili na kutoa maoni.

Suluo amesema LATRA wamekuwa wasimamizi katika sehemu kuu tatu za reli,barabara na waja hili likiwa eneo jipya lipo kwenye mchakato
“Katika suala hili LATRA imepewa mapendekezo na TRC na tumeyapokea na kuyaleta kwanu kama wadau. ili mtoe mapendekezo yenu kwa maslahi ya pande zote’’anasema.

Safari yetu ya kukusanya maoni kwa wadau hapa Dar es Salaam itakuwa kwa njia ya mkutano huu na njia za kutuma maoni katika taasisi yetu kupitia barua pepe na barua mpaka tarehe 30 mwezi huu.

Amesema baada ya hapo wanatarajia kwenda mikoa mingine likimalika zoezi la Sensa kukusanya maoni kwa wadau wengine.

Zoezi hili ni la kisheria na litakwenda kwa utaratibu wa kufuata ngazi mbalimbali, mpaka kufikia hatua ya kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali kwa ajili ya utekelezaji

By Jamhuri