Na Mussa Augustine,JamhuriMedia

Mashindano ya Dunia ya Mister and Miss Kiziwi yanatarajia kufanyika oktoba 29 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Kimatataifa( NJICC) na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu,nakwamba yanakutasha washiriki kutoka nchi 47 Duniani.

Akizungumza na Waandishi wa habari Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas amesema kuwa Tanzania imepewa heshima kubwa yakuwa mwenyeji wa mashindano hayo yanayofanyika Oktoba 29 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri.

Dkt Hassan Abasi kulia akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kuelekea mashindano ya kidunia ya Mister na Miss Kiziwi yanafanyika Oktoba 29 mwaka huu,kushoto ni rais wa Viziwi Afrika Habibu Mlope

Aidha amesema kuwa mejaji kutoka nchi mbalimbali wameshawasili nchini Tanzania huku washiriki wapatao 400 wanatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo.

‘” Tumepewa heshima kubwa, nasisi kama serikali tumelichukulia Kwa uzito suala hili ,tunatarajia wageni elfu moja mianne watakaohudhulia,hivyo nawaomba wale wote walioalikwa wajitokeze Kwa wingi ili kufanikisha mashindano haya” amesema.

Aidha amewasihi washiriki wa mashindano hayo kutambua kuwa kunakuwhindwa na kushinda hivyo wawe wastaarabu kupokea matokeo kutoka kwa majaji kwani hadi kufikia hatua yakupeperusha bendera za nchi zao kuja Tanzania kushiriki wamefanya Mambo makubwa katika ushiriki wao.

Dkt Abbas amesema kuwa washindi wa shindano Hilo watapsta fursa yakutembelea hifadhi ya ngolongolo nakufanya Utalii ambapo hatua hiyo ni sehemu yakuitangqza Tanzaia katika sekta ya Utalii.

Rais wa Viziwi Afrika Habibu Mlope( aliyenyanyua mikono) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es salaam kuelekea mashindano ya ya kidunia Mister na Miss Kiziwi Oktoba 29 mwaka huu

Kwa upande wake rais wa Dunia wa Viziwi Bonita Annleek ameishukuru serikali ya Tanzani Kwa kufanya maandalizi mazuri ya mashindano hayo huku alisisitiza kuwa wataendeleza mahusiano mazuri kati ya nchi ya Tanzania na Nchi zingine.

“Nimefurahi sana kuona Tanzania inajari kundi hili la viziwi, kwakuwekeza fedha kuweza kufanikisha mashindano haya yakidunia,Oktoba 31.2022 washindi wamepata fursa yakwenda kutembelea Hifadhi ya ngorongoro mara baada ya mashindano haya kumalizika hivyo fursa hii ni muhimu kwao na waitumie” amesema Bonita.

Nae raisi wa Viziwi Afrika Habibu Mlope amesema kwamba awamu hii ni mara ya pili Tanzania kushiriki Mashindano ya Mister and Miss Kiziwi hivyo haina budi kuishukuru serikali ya raisi Samia Suluhu kwa utendaji wake uliotukuka.

Baadhi ya Washiriki wa mashindano hayo wamebainisha kuwa wamefanya maandalizi yakutosha nakwamba wapo tayari kupanda jukwaani na kushiriki Mashindano hayo.

By Jamhuri